ABOUT US



CHILDREN ON THE EARTH FOUNDATION (CEF)
P.O. BOX 72, KASULU -  KIGOMA
Phone:  +255 767325090/+255 756606087/+255 719744411

CEF NA SHUGHULI ZAKE
Children on Earth Foundation (CEF)
CEF ni Shirika lisilo la Kiserikali la Kulinda na Kutetea Haki za Watoto Tanzania. Makao Mkuu ya Shirika hili yapo Kasulu Kigoma. Shirika linatambulika kiserikali na limesajiliwa kwa namba 06NGO/00005955 chini ya kifungu cha Sheria No.24 ya mwaka 2002 tarehe 26 Novemba 2012.
Lengo Kuu.
Kuwa na jamii yenye maisha bora na mazingira safi na salama kama ukombozi kwa afya ya watoto na mahitaji yao ya lazima.
Malengo mengineyo.
Ø  CEF inalenga kuanzisha shule ya watoto yatima, watoto wa mitaani na watoto wasiojiweza. Hii ni pamoja na watoto walemavu.
Ø  CEF inalenga kuanzisha Kituo cha Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kulea watoto yatima.
Ø  CEF ina mwanasheria anayesimamia sheria ya mtoto pindi unapotokea uvunjifu wa sheria hiyo (ukatili).
Ni pamoja na kufuatilia kesi zote zinazowahusu watoto kuanzia polisi, mahakamani hadi watoto walioko magereza.
Shughuli za CEF (Kutoa Elimu kwa jamii na Kusimamia yafuatayo)
·         HAKI ZA BINADAMU
·         HAKI ZA WATOTO TANZANIA

Ø  Elimu bora na maadili shuleni
Ø  Lishe bora kwa jamii
Ø  Afya na mazingira safi na salama ya mama na mtoto
Ø  Michezo na burudani (kuibua vipaji)
Ø  Kufuatilia kesi zote zinazowahusu watoto polisi, mahakamani na magerezani ili kuona na kuhakikisha haki ya mtoto inatendeka kwa kutumia mwanasheria wake.
Ø  Kuwapa wazee, vikongwe na wajane msaada wa mahitaji muhimu kama vile chakula na mavazi
Ø  Kuwapatia msaada wa tiba watoto wenye magonjwa sugu.
Ø  Kutoa msaada kwa watoto walemavu wa viungo, ngozi, akili, watoto yatima, watoto waliotekezwa, watoto wa mitaani na waathirika wa HIV (UKIMWI)

Njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii.
Ø  Semina, warsha na mikutano
Ø  Vipeperushi, mabango, t-shirt, gazeti na redio
Ø  Michezo na burudani

CEF  INALENGA MAKUNDI YAFUATAYO,
Ø  Watoto walioko chini ya umri wa miaka 18
Ø  Mama mjamzito na mama anayenyonyesha
Ø  Watoto wa mitaani, yatima na waliotelekezwa na wazazi wao
Ø  Walemavu wa ngozi, viungo na akili
Ø  Watoto waishio katika mazingira hatarishi
Ø  Waathirika wa HIV (UKIMWI) na madawa ya kulevya
Wazee, vikongwe n

No comments:

Post a Comment